WORLD SOLUTION

WORLD SOLUTION
full

best news best news best temlates best templates best templates best news best news

Subscribe For Free Updates!

We'll not spam mate! We promise.


EDITING BADO ZINAENDELEA.-- USIACHE KUTEMBELEA BLOG YETU ANGALAU MARA 1 KWA SIKU HAKIKA UTAKUA WA TOFAUTI.-- ENDELEA KUFURAIA BLOG YETU.
#htmlcaption1 Go UP! Pure Javascript. No jQuery. No flash. #htmlcaption2 Stay Connected

Friday, 12 July 2013

MARUFUKU KUMUUZIA POMBE GAZZA


WITO WATOLEWA UINGEREZA: MARUFUKU KUMUUZIA POMBE "GAZZA" ATAKUFA

GAZETI la The Sun la Uingereza limeanzisha kampeni maalumu ya kunusuru maisha ya ‘chapombe’ Paul Gascoigne “Gazza” kwa kuwataka wamiliki wa baa na maduka kukataa kumuuzia pombe.
Pia limewataka marafiki zake, mashabiki wa soka au mtu yeyote awaye kuacha kumnunulia pombe staa huyo wa zamani ili kusaidia kuokoa maisha yake.
Gazza, 46, alilazimika kupelekwa hospitalini wiki hii baada ya ‘kuzimika’ kwa kilevi nje ya hoteli moja jijini London, huku akiwa akiwa na chupa nyingine mbili za pombe kwenye mifuko yake.
Kiungo huyo wa zamani wa Newcastle, Spurs, Everton, Rangers na timu ya taifa ya Uingereza alipigwa picha na The Sun juzi akiwa chakari akijaribu kujiinua karibu na pipa la takataka nje ya hoteli hiyo.

Gazza, akiwa na magongo ya kutembelea, baadae alinaswa na kamera za CCTV akigida chumba ya pombe akiwa amesimama katika duka moja jijini London.

Gwiji huyo alianza tena kukata kilevi baada ya kufanyiwa operesheni ya nyonga mwezi uliopita.
Alishikiliwa na polisi wiki iliyopita kwa madai ya kumshambulia mke wake wa zamani, Sheryl kwenye stesheni ya reli ya Stevenage huko Herts akichagizwa na ulevi.

Ni karibu miaka 15 sasa Gazza amekuwa akipambana na ulevi wa kupindukia tangu alipoanza kupata tiba ya kumrejesha katika hali ya kawaida baada ya kunywa chupa 32 za whisk mwaka 1998.

Please Give Us Your 1 Minute In Sharing This Post!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

1 comments: