WITO WATOLEWA UINGEREZA: MARUFUKU KUMUUZIA POMBE "GAZZA" ATAKUFA
GAZETI la
The Sun la Uingereza limeanzisha kampeni maalumu ya kunusuru maisha ya
‘chapombe’ Paul Gascoigne “Gazza” kwa kuwataka wamiliki wa baa na maduka
kukataa kumuuzia pombe.
Pia
limewataka marafiki zake, mashabiki wa soka au mtu yeyote awaye kuacha
kumnunulia pombe staa huyo wa zamani ili kusaidia kuokoa maisha yake.
Gazza,
46, alilazimika kupelekwa hospitalini wiki hii baada ya ‘kuzimika’ kwa
kilevi nje ya hoteli moja jijini London, huku akiwa akiwa na chupa
nyingine mbili za pombe kwenye mifuko yake.
Kiungo huyo
wa zamani wa Newcastle, Spurs, Everton, Rangers na timu ya taifa ya
Uingereza alipigwa picha na The Sun juzi akiwa chakari akijaribu
kujiinua karibu na pipa la takataka nje ya hoteli hiyo.
Gazza,
akiwa na magongo ya kutembelea, baadae alinaswa na kamera za CCTV
akigida chumba ya pombe akiwa amesimama katika duka moja jijini London.
Gwiji huyo alianza tena kukata kilevi baada ya kufanyiwa operesheni ya nyonga mwezi uliopita.
Alishikiliwa
na polisi wiki iliyopita kwa madai ya kumshambulia mke wake wa zamani,
Sheryl kwenye stesheni ya reli ya Stevenage huko Herts akichagizwa na
ulevi.
Ni karibu
miaka 15 sasa Gazza amekuwa akipambana na ulevi wa kupindukia tangu
alipoanza kupata tiba ya kumrejesha katika hali ya kawaida baada ya
kunywa chupa 32 za whisk mwaka 1998.
photoshop cs6 extended serial key
ReplyDelete