Watu zaidi ya 75 wamekufa nchini Hispania kufuatia ajali mbaya ya treni kuacha njia na kupinduka.
Watu
takriban 75 wamekufa na wengine zaidi ya 120 kujeruhiwa kati ya abiria
200 baada ya treni moja ya abiri kuacha njia na kuanguka kaskazini
magharibi mwa Hispania.
Mabehewa yote 8 ya treni hiyo iliyokuwa ikitoka Madrid kuelekea Ferrol yameanguka karibu na mji wa Santiago de Compostela.
Taarifa
za vyombo vya habari zinasema huenda treni hiyo ilikuwa ikienda kwa
mwendo kasi wa mara mbili ya kipimo chake katika eneo lenye kona.
Maafisa
mjini humo hawajasema lolote kuhusiana na chanzo cha ajali hiyo huku
wachambuzi wa mambo wakisema ni ajali mbaya zaidi ya treni kutokea
nchini Hispania katika kipindi cha miaka 40.
Ajali
kubwa ya treni kuwahi kutokea nchini humo ilikuwa mwaka 1972 wakati
watu 77 walipokufa baada ya treni kuacha njia huko Andalusia eneo la
kusini.
0 comments:
Post a Comment