Tibaasili ya Ukimwi yaiduwaza NIMR
TAASISI ya Taifa ya Utafiti wa Dawa za Binadamu (NIMR), imepokea dawa
asili ambayo sasa inaonesha matumaini mazuri katika kukabiliana na virusi
vinavyosababisha upungufu wa kinga mwilini (Ukimwi).
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa
Kuratibu Utafiti wa taasisi hiyo, Dk Julias Massaga, alisema NIMR inaifanyia
utafiti wa kina dawa hiyo, kwa sababu imeonesha matumaini mazuri katika ugonjwa
huo.
"Kuna waganga watatu walileta dawa zao kwa ajili ya utafiti wakidai
zinatibu ugonjwa wa Ukimwi, moja ilikuwa katika hali ya unga lakini sasa
tumeitengeneza katika vidonge na tunaendelea nayo na utafiti kwa kuwajaribu
wagonjwa," alisema.
Waganga hao walikubali dawa zao kufanyiwa utafiti, baada ya kutengeneza
mikataba nao, ndipo ikajulikana nguvu yake. Dk Massaga alisema dawa hiyo
inayodaiwa kutibu ugonjwa wa Ukimwi, ambao kwa miaka mingi sasa hauna tiba wala
kinga, imeleta manufaa kidogo na hivyo watakwenda nayo mbali katika uchunguzi.
Hata hivyo, Dk Massaga alisema tiba asili imevamiwa na matapeli wengi,
hasa katika miji mikubwa, ambapo waganga hudanganya watu kuwa wanatibu magonjwa
mbalimbali, kumbe wanataka kujipatia fedha.
Nchi nyingi kama Asia kwa mujibu wa Dk Massaga, madaktari wa sayansi na
wale wa jadi, hushirikiana katika matibabu kwa sababu huduma na dawa zao
zimeboreshwa katika kiwango cha juu.
Mwaka huu, NIMR ina mpango wa kusajili dawa za jadi, jambo ambalo Dk
Massaga alisema lilishindikana kwa sababu hawakuwa na mtambo wa uzalishaji wa
dawa zenye ubora.
"Watu wanakosa imani na dawa za jadi kwa sababu hazina vipimo
sahihi vinavyotambuliwa, lakini sasa tunaboresha na kuweka vipimo baada ya
kuzifanyia utafiti dawa na kuwa na uhakika nazo," alisema Dk Massaga.
Alisema Serikali imejenga maabara na kiwanda cha kisasa cha daraja la
kwanza, kwa ajili ya utafiti na utengenezaji wa tiba za asili katika eneo la
Mabibo jijini Dar es Salaam, ambapo Sh milioni 800 katika mwaka huu wa fedha
zimetengwa kwa ajili ya kumalizia ujenzi na kununua mitambo.
Changamoto nyingine katika kuaminiwa kwa dawa hizo, kuwa ni mitaala ya
wataalamu wa tiba ya sasa, kutoelewa kwa kina juu ya tiba za asili, matumizi
yake na vipimo vya tiba hizo. Nyingine ni kutokuwepo kwa orodha ya miti yenye
dawa, taarifa ya matumizi yake katika tiba, na muingiliano wa dawa za kisasa na
za asili katika mfumo wa tiba.
Dk Massaga alisema taasisi hiyo imefanikiwa kutengeneza tiba asili
zilizoboreshwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu, ikiwa ni pamoja na tiba za
malaria, ini, magonjwa nyemelezi, kisukari, tezi dume, kikohozi na mafua,
kuongeza nguvu za kiume na tiba ya maji ya kunywa.
Wakati huo huo, NIMR imesema iko katika utafiti kubaini kama mafuta ya
ubuyu yana sumu au la, kama ilivyoelezwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).
TFDA katika taarifa ya hivi karibuni, iliwataka Watanzania kuacha
kutumia mafuta ya ubuyu kwa kunywa, kwa kuwa yana tindikali ya mafuta, ambayo
husababisha saratani za aina nyingi.
Mamlaka hiyo ilisema kuwa hawana tatizo na majani na unga wa ubuyu
kutumika kwa kula, na hata mafuta hayo yakitumika kwa kupaka katika ngozi kama
kipodozi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya TFDA, ili mafuta hayo yawe salama, lazima
tindikali hiyo itolewe, lakini ikaonya kuwa Tanzania hakuna teknolojia ya
kutenganisha tindikali hiyo na mafuta hayo.
cracked adobe photoshop
ReplyDeleteTibaasili Ya Ukimwi Yaiduwaza Nimr ~ 1 World Solution >>>>> Download Now
ReplyDelete>>>>> Download Full
Tibaasili Ya Ukimwi Yaiduwaza Nimr ~ 1 World Solution >>>>> Download LINK
>>>>> Download Now
Tibaasili Ya Ukimwi Yaiduwaza Nimr ~ 1 World Solution >>>>> Download Full
>>>>> Download LINK