WAZIRI wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe amesema
haoni msingi wa wasafiri kulipa kiingilio cha sh 200 kwenye Stendi kuu ya
Mabasi yaendayo mkoani cha Ubungo (UBT).
Alisema jana hafurahii hali wanayokutana nayo wasafiri
wanaotumia kituo hicho kutokana na kubomolewa vibanda vilivyokuwa vikiwasaidia
kujihifadhi kwa lengo la ujenzi wa mradi wa mabasi yaendayo kasi.
Dk Mwakyembe ambaye ameahidi kukutana na wahusika
kufanyia kazi suala hilo, alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumza na
waandishi ambao pamoja na maswali mbalimbali, walitaka kufahamu msimamo wake
kuhusu hali ya kituo hicho.
“Sifurahii suala hilo…ni changamoto kubwa kwangu
lakini nitawasiliana na ofisi ya Waziri Mkuu ambao ndio wanaofuatilia
utekelezaji wa mradi huo wa mabasi ya kasi,” alisema Dk. Mwakyembe na
kusisitiza hali ilivyo kituoni hapo ni kero na hakuna haja ya kulipa ushuru
huo.
Kwa sasa katika kituo hicho kikuu cha mabasi, wasafiri
wamekuwa wakihangaika kupata sehemu ya kujihifadhi kutokana na kubomolewa kwa
mabanda.
Kabla ya kituo hicho kubomolewa, uongozi wa
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ulikuwa umesema Mei mwaka huu kituo hicho
kingekuwa kimehamishiwa eneo la Mbezi Luis jambo ambalo hadi sasa
halijatekelezwa.
photoshop free serial number
ReplyDelete